Breaking News
Loading...

Created with flickr slideshow.

Recent Post

Friday, February 6, 2015
BOBBY BROWN AKATAA USHAURI WA MADAKTARI. ASEMA UHAI WA MWANAE UPO CHINI YA MUNGU

BOBBY BROWN AKATAA USHAURI WA MADAKTARI. ASEMA UHAI WA MWANAE UPO CHINI YA MUNGU

Mkali Bobby Brown amekataa wazo la madaktari wanao mtibu mwanae Bobbi Kristina la kumtolea mitambo ya kumsaidia kupumua.
Hatua hiyo ilikuja baada ya madaktari kushauri kuwa ni vyema kumtolea hizo mashine tu kwani hakuna matumaini ya kupona. Lakini Baba, Bobby Brown amesema kuwa hawezi kuruhusu kutolewa hizo mashine, amedai kuwa uhai wa mwanae unamtegemea mungu.
Kimsingi Bobbi yupo kwenye hard time na anahitaji support kubwa kwa sasa.
Sunday, December 21, 2014
Mshindi wa Pili BBA 2014, Tayo Faniran azidi kufanyiwa mambo makubwa

Mshindi wa Pili BBA 2014, Tayo Faniran azidi kufanyiwa mambo makubwa


Tayo Faniran ni jina lililovuma sana katika jumba la Kaka Mkubwa 'Big Brother' Africa 2014. Licha kwamba alikuwa na kaumaarufu fulani kikwaokwao lakini kwa nchi zingine tumemjua kupitia BBA 2014. Ndio, alikuwa hajulikani kwetu. Alikuwa ni mshiriki kutoka Nigeria, mtu mwenye misimamo, mcheshi pia very social kwa kipindi chote alichokuwa BBA.
Tayo mwisho wa siku alifanikiwa kuwa mshindi wa pili katika safari ya BBA, na mshindi wa Kwanza alikuwa kaka yetu wa Ukaye, Idris Sultan ambapo alijinyakulia kitita cha dola za kimarekani laki tatu ($300,000).
Lakini Tayo ameweza kufanyiwa mambo makubwa na mashabiki wake ukilinganisha na mshindi wa kwanza. kitu cha kwanza kabisa baada ya kutangazwa kushika nafasi ya pili, Milionea wa Nigeria Ayiri Emami ametangaza kumpatia Tayo dola za kimarekani laki tatu na hamsini ($350,000) ikiwa imezipita hadi zile za mshindi wa kwanza. Pia jana tarehe 20/12/2014 amefanyiwa party kubwa ya kukaribishwa nyumbani akitokea South Africa alikokuwa anafanya reality show kwa kipindi chote baada ya BBA.
Mbali na hilo jamaa wanajiita @malivelihood wamemfanyia customization ya limited edition ya Iphone 6. Kwaujumla jamaa katisha sana.
Touch me- A.Y feat. Sean Kingston & Ms. Trinity (Official Video)

Touch me- A.Y feat. Sean Kingston & Ms. Trinity (Official Video)

Ambwene Yesaya, muite A.Y, ni msanii wa bongo ambaye anapenda anachokifanya. Ni mmoja kati ya wasanii ambao wanaitangaza Tanzania katika anga za kimataifa. Hapa yupo na Wakali wawili, Sean Kingston na Ms. Trinity, Ngoma inaitwa Touch me. Enjoy.
Joh Makini feat. G. Nako- XO 'Official Video'

Joh Makini feat. G. Nako- XO 'Official Video'

Ni ngoma kali, na Joh Makini akiwa na Mweusi G. Nako wamefanya yao,iko poa. Kikubwa Nisher katisha kwa shots kali, colour na vitu kamahivyo.Huwa napenda kuwaongelea Weusi kuwa wako serious na kazi zao. Big up!

Alikiba- Mwana 'Official Video'

Alikiba- Mwana 'Official Video'

Ali Kiba amerudi upya, wimbo wake wa mwana ndo unamuweka pazuri kwa ujio huu. Hii ni official video ya wimbo wa Mwana. kwa mtazamo wangu sio mbaya, shots nzuri, rangi nzuri, lakini stori na location sijapenda  sana. All in all kazi nzuri.
Huyu ndo Miss World 2014, Rolene Strauss kutoka South Africa

Huyu ndo Miss World 2014, Rolene Strauss kutoka South Africa


Baada ya kushinda taji la ulimbwede wa dunia, Rolene Straus amerejea kwao Afrika ya Kusini na kupokelewa kwa mbwembwe za kutosha. Kimsingi Rolene ameshinda taji hilo Jumapili iliyopita mjini london uingereza akiwashinda washiriki 120.

Mshiriki wetu wa bongo Bi. Happiness Watimanya ametuwakilisha vizuri ingawa bahati haikuwa ya kwake. Japo angalau Ameweza kuingia Top ten ya 'The People's Choice'. Afrika JUU!
Diamond na Zari sasa mambo hadharani, cheki mapicha wakijiachia..

Diamond na Zari sasa mambo hadharani, cheki mapicha wakijiachia..

Kwa Lugha rahisi naweza kusema kuwa Dada yetu Wema hana chake tena kwa Mkali Diamond kwani tayari Bi dada Zari keshajiweka na kuchanua vilivyo kwa mkali huyu wa bongo flavour.
Zari 'The Bosslady' Tlale juzi kati katika party yake ya 'Zari All White', ameamua kuonesha wazi kuwa kwasasa yupo na Diamond Platinumz kwa kujiachia mbaya na mkali  'shemeji wetu wa zamani'.
Jionee mapicha yao wakiwa wamejiachia kimpango wao.




Back To Top